+255(0)232604380/1/3/4 | P.O. Box 9, Mzumbe, Morogoro - Tanzania

Mar 30, 2023 268times

VIONGOZI MZUMBE WATAHADHARISHWA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe, leo imepokea mafunzo kuhusu namna ya uendeshaji wa Dawati la Jinsia, na kujengewa uwezo wa namna darati hilo linavyofanya kazi na kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia unaoweza kutokea chuoni hapo.

Mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika Kampasi Kuu Morogoro, yametolewa na maafisa kutoka Wizara ya Maendeleo ya JamiiJinsia Wanawake na Makundi Maalum, Idara ya Ustawi wa Jamii, ambapo pamoja na mambo mengine mafunzo hayo yamesisitiza elimu kuhusu unyayasaji wa kijinsia na kuzuia vitendo vya ukatili kwa wafanyakazi, wanafunzi na watoa huduma.

Akizungumza wakati wa kuwakaribisha maafisa hao, Prof. Allen Mushi, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala, akimwakilisha Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, amesema, mafunzo hayo ni muhimu katika kuleta uelewa wa pamoja kwa Menejimenti, Wafanyakazi na Wanafunzi, hususani katika kipindi hiki chuo kinapokwenda kuzinduliwa rasmi dawati la Jinsia chuoni hapo ambalo litakuwa na wajibu wa kisheria na kikanuni katika kushughulikia changamoto na matukio yote ya unyanyasaji wa kijinsia utakaokuwa ukitokea chuoni hapo.

Naye mkufunzi Bw. John Mapunda amesema, Wizara imekusudia kufuatillia kwa karibu  ufanisi wa madawati ya Jinsia yanayoanzishwa katika Taasisi za Elimu ya Juu, na namna yanavyoshughulikia changamoto na vitendo vya kikatili vitakavyokuwa vikiripotiwa na wadau mbalimbali ambao ni walengwa katika mwongozo uliotolewa na Wizara hiyo katika kushughulikia, kudhibiti na kukomesha vitendo vya kikatili  na  unyanyasaji wa kijinsia kwenye Taasisi za Elimu ya Juu.

“Tunategemea Dawati hili kufanya kazi ya kuelimisha zaidi ili kupunguza na kutatua changamoto za viashiria vya kufanyika kwa vitendo vya kikatili, badala ya kusubiria kuripotiwa matukio ambayo tayari yamelewa madhara na athari kwa wahanga” alisema

Mafunzo hayo ya siku moja yameanza na Menejimenti ya Chuo na baadae yatafanyika kwa wafanyakazi na wanafunzi wa Kampasi Kuu, kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa dawati la Jinsia, Alhamisi ya tarehe 23 Machi 2023.

Kwa mujibu wa Prof. Mushi, mafunzo hayo yatafanyika Kampasi zote, na madawati katika kila Ndaki kuzinduliwa, ili kuendana na matakwa ya mwongozo wa Wizara wa kuanzisha madawati hayo, kushugulikia na kudhibiti vitendo vyote vya Ukatili wa kijinsia vinavyoweza kutokea vyuoni.

 

Mratibu wa Dawati la Jinsia la Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Khanifa Massawe akichangia jambo wakati wa mafunzo ya Menejimenti ya Chuo.

Bw. Emmanuel Makita, mmoja wa wakufunzi kutoka Wizara Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na

Makundi Maalum, Idara ya Ustawi wa Jamii akitoa ufafanuzi wa jambo kwa washiriki wa mafunzo.

Mkufunzi katika mafunzo ya Menejimenti kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Idara ya Ustawi wa

Jamii, Bw. John Mapunda akionyesha rejesta ya kujaza matukio yatakayokuwa yakiripotiwa kwenye Dawati la Jinsia lililoanzishwa Chuo Kikuu Mzumbe.

Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti wakisikiliza kwa makini mafunzo kuhusu uanzishwaji wa Dawati la Jinsia Chuo Kikuu Mzumbe

Go to top
JSN Educare is designed by JoomlaShine.com | powered by JSN Sun Framework