+255(0)232604380/1/3/4 | P.O. Box 9, Mzumbe, Morogoro - Tanzania

Jun 28, 2022 75times

WASOMI WAHIMIZWA KUANDAA MIJADALA YA KITAALUMA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka amewataka Wanataaluma wa chuo kikuu Mzumbe kuandaa kwa wingi mijadala ya uwasilishaji wa makala za kitaaluma Chuoni hapo kwani ni chachu ya kukuza ujuzi na uelewa wa masuala mbalimbali katika jamii.

 Prof. Lughano Kusiluka amesema hayo wakati wa uwasilishaji wa makala za kitaaluma uliofanyika Chuo Kikuu Mzumbe kupitia  Kitivo cha sheria mwishoni wa wiki, ambapo aliwaagiza wakuu wa vitivo kupata mwamko wa kuandaa mijadala ya kitaaluma kwani ndio inayoipa hadhi na tafsiri sahihi ya kuitwa Chuo Kikuu.

 “Nina furaha kuwa hapa leo, na mara zote nitahakikisha nashiriki mijadala hii kwani ndio inayoleta dhana ya kuwa Chuo Kikuu, lakini pia tutahakikisha mijadala hii kwenda mbali zaidi. Alisisitiza.

 Aidha, amewataka wanajumiya wa Chuo Kikuu Mzumbe kushiriki kwa wingi katika mijadala hiyo ili kukuza uelewa wa mambo ya kitaaluma na kijamii.

 Kitivo cha sheria kiliandaa mjadala wa uwasilishaji wa makala za kitaaluma ili kuongeza uelewa wa  mambo ya kisheria ambapo mtoa mada wa kwanza alikuwa ni nguli wa Sheria nchini Prof. Cyriacus Binamungu, aliyetoa mada ya “ Miaka 50 ya sheria ya Ndoa” akiangazia,  maendeleo na changamoto za kisheria, akifuatiwa na Dkt. Mwajuma Kadilu Juma,aliyewasilisha mada ya “Elimu na malengo endelevu” akiangazia, changamoto za kisheria kwa watoto wanaopata ujauzito.

 

Prof. Cyriacus Binamungu, akiwasilisha mada kuhusu Miaka 50 ya sheria ya Ndoa akiangazia, maendeleo na changamoto za kisheria, katika uwasilishaji

wa makala za kitaaluma za  sheria uliofanyika  katika ukumbi wa Fanon Kampasi kuu, Mzumbe,Morogoro.

 

Wanataaluma na Wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe wakisikiliza na kufuatilia uwasilishaji wa makala za kitaaluma.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka akisilikiza uwasilishaji wa makala za kitaaluma za Sheria uliofanyika katika ukumbi wa Fanon

Kampasi kuu, Chuo Kikuu Mzumbe,Morogoro.

Go to top
JSN Educare is designed by JoomlaShine.com | powered by JSN Sun Framework