+255(0)232604380/1/3/4 | P.O. Box 9, Mzumbe, Morogoro - Tanzania

Jan 28, 2022 941times

Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo

Chuo Kikuu Mzumbe kupitia Kitivo cha Sheria Kwa ushirikiano na Chama cha wanafunzi wanasheria Cha Chuo Kikuu Mzumbe, wameendesha mafunzo kwa vitendo kwa kuandaa mahakama ya mafunzo "Moot Court" iliyowahusisha wanafunzi wa Sheria kutoka  Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu Cha Jordan. Miongoni mwa walioalikwa kushuhudia mahakama hiyo  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha, wahadhiri na wanasheria nguli. Kwa mujibu wa mratibu wa mafunzo hayo Bw. Deogratius Mapendo wa Chuo Kikuu Mzumbe, amesema kitaalamu mafunzo hayo yanajulikana kama "Inter University Moot court" ambayo yanalenga kuwaandaa vema wahitimu katika kufahamu taratibu za mashauri mahakamani, kujenga hoja na kutetea hoja Kwa kutumia vifungu vya Sheria pamoja na kuwajengea uwezo wa kujiamini wanapotekeleza wajibu wao mahakamani. Mafunzo hayo yamefanyika sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini, ambapo huduma na misaada mbalimbali ya kisheria imeendelea kutolewa kwa wananchi kote nchini kwa ngazi mbalimbali.

Picha hapo chini ni za matukio mbalimbali kwenye hayo Mafunzo.

 

 

 

 

Go to top
JSN Educare is designed by JoomlaShine.com | powered by JSN Sun Framework