+255(0)232604380/1/3/4 | P.O. Box 9, Mzumbe, Morogoro - Tanzania

Sep 28, 2020 3914times

MAONESHO YA 15 YA VYUO VIKUU 2020

BANDA la Chuo Kikuu limekuwa kivutio kikubwa katika maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu yaliyoanza leo viwanja vya viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Hii ni kutokana na wingi wa programu na ubobevu katika ufundishaji baada ya dirisha la udahili kufunguliwa rasmi.Kozi hizo zitakuwa zinafundishwa katika Kampasi zake zilizopo Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam kwa ngazi ya Stashada, Astashahada, Shahada za Kwanza na Shahada za Uzamili.

 Sambamba na hilo Chuo hicho kimesha masomo ya Shahada za Awali Kampasi ya Dar es Salaam, Tawi la Tegeta ambazo zitaanza rasmi mwaka wa masomo 2020/2021.Kozi hizo ni " Bachelor of Public Administration (BPA) na Bachelor of Accountancy and Finance- Business Sector (BAF-BS)."

 Wakizungumza wakati wa usajili baadhi ya wanafunzi wamesema wameamua kijiunga na chuo hicho kutokana na ubora wake katika ufundishaji na kuzaliwa wanataluma wabobevu katika sekta mbalimbali.

 "Huduma za Banda la Chuo Kikuu Mzumbe ni nzuri kwani wanakushauri na kukuelekeza vizuri kuhusu kozi bora za kisoma kulingana na ufaulu wako' alisisitiza, Amina Omary.

Chuo Kikuu Mzumbe ni miongoni mwa Chuo Kikuu cha Umma kinachotoa Elimu ya Juu nchini kikiwa na zaidi ya wanafunzi 11,000 nchi nzima.

      KUFANYA MAOMBI CHUO KIKUU MZUMBE,BOFYA HAPA

Go to top
JSN Educare is designed by JoomlaShine.com | powered by JSN Sun Framework