Print this page
Jun 03, 2019 6516times

CHUO KIKUU MZUMBE CHATOA MZUNGUMZAJI BORA MASHINDANO YA SHERIA KIMATAIFA

Chuo Kikuu Mzumbe kupitia kitivo cha Sheria kimeendeleza rekodi ya ushindi ambapo mwaka jana Kampasi yake ya Mbeya ilitinga fainali ya mashindano ya ICRC-International Humanitarian Law, National Moot Court Competition ambayo hufanyika kila mwaka na kushirikisha Vyuo Vikuu vinavyofundisha somo la sheria za kimataifa zinazolinda watu nyakati za vita (Law of War),mwaka huu Pia Chuo Kikuu Mzumbe kimeshiriki mashindano hayo na kuwakilishwa na timu toka Campus ya Mbeya na Main campus. Jumla ya Vyuo 12 vilishiriki katika mashindano. Baadhi ya vyuo hivyo ni Mzumbe University Morogoro, Mzumbe University Mbeya Campus, Tumaini University-Makumira, Tumaini University-Dar es salaam, Ruaha College, Stella Maris Mtwara, SAUTI Mwanza, Zanzibar University, UDSM, UDOM, SAUTI MBEYA.

Chuo Kikuu Mzumbe-Main Campus kilifanikiwa kutinga nusu fainali na kupambana na Ruaha University na kuwatoa na hatimaye kutinga fainali walipokutana na UDOM. Katika fainali UDOM waliibuka kidedea lakini mshiriki kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, David Mtanke (mwaka wa tatu) amechaguliwa kuwa Mzungumzaji bora (Best Speaker) katika mashindano hayo.

Kufuatia ushindi huo, UDOM sasa wamepata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya East Africa yatakayofanyika Arusha baadae mwaka huu.